“Our Congregation dedicates itself to the needs of the local and universal Church and devotes itself the Parrochial ministry and other works of the Apostolate which are assumed according to the Provincial, Vicariate and the norms of the Mission.” (NT S11)
OUR MISSION HOUSES
Below are our houses, click on the name to view
Parokia ya Mt. Yuda Tadei ipo eneo linaloitwa Gunyoda, katika halmashari ya mji wa Mbulu. Ni kilomita 13 toka mjini Mbulu. Parokia hii ilizaliwa mwaka 2004 toka Parokia ya DAWDI ambapo waliinjilishwa na kuhudumiwa na shirika la Ndugu wadogo Wakapuchini (OFM Cap). Parokia ilipozaliwa ikaanza kuhudumiwa na mapadre wa Jimbo kwa ushirikiano na mapadre Wakapchini OFM Cap. Tulipowasili hapa katika macho ya wakristo na viongozi walei ni kama usiku mrefu umekwisha, jua limechomoza. Wamekuwa na shauku kubwa kuona mabadiliko yanatokea. Ni watu wazuri wenye imani na rasilimali nyingi. Shida kubwa waliopata ni kukosa Mchungaji wa kuwasikiliza, kuwaongoza na kuwahamasisha hasa ukizingatia sehemu kubwa ni wafugaji na wanajua mchungaji ni nani. Parokia ina vigango 11 vilivyounganishwa na kutengeneza kanda tatu (3) ili kurahisisha huduma. Na kanda zote hizi zina makanisa yenye Ekaristi takatifu ndani na nyumba ya Padre. Idadi ya wakristo ni zaidi ya 4,000/- Makabila ya hapa ni Wairaqw, Wamang’ati na kabila ndogo la Wahdzabe. Hitaji kubwa kwa sasa ni Uinjilishaji na uhamasishaji wa shughuli nyingine za maendeleo. Wakristo wana kiu kubwa ya huduma za kiroho ambapo inahitaji mapadre angalau wawili kwa uchache. Ndoto ya Mt. Gaspari del Bufalo, Inaendelea.