MISSION HOUSES


“Our Congregation dedicates itself to the needs of the local and universal Church and devotes itself the Parrochial ministry and other works of the Apostolate which are assumed according to the Provincial, Vicariate and the norms of the Mission.” (NT S11)

Benaco Rulenge Ngara

Parokia ya Mt. Josephina Bakhita-Benaco ilitangazwa parokia teule mnamo Mei, 2011 na kuzinduliwa rasmi kuwa parokia tarehe 10/03/2017. Parokia hii ina vigango 15, kati ya hivyo ni vigango 8 tu vinavyofikika kwa gari muda wote, vilivyobaki ni kwa njia ya pikipiki tu, na wakati wa mvua utume husimama hadi kiangazi. Hali za vigango zinatofautiana kulingana na mazingira na watu wanaounda vigango hivyo. Benaco ni eneo linaloundwa na watu toka sehemu mbalimbali. Hii inatokana na historia ya kuundwa kwake. Kabla ya mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994, eneo hili lilikuwa kwa sehemu kubwa ni pori. Lakini baada ya wakimbizi kupata hifadhi maeneo haya watu toka sehemu mbalimbali walihamia hapa kwa lengo la kujipatia fursa. Baada ya wakimbizi kurudi makwao wengi wa makundi haya walibaki na kuendelea na shughuli za biashara, kilimo na ufugaji.

Miundo mbinu ya vigango ni hafifu kwani yapo makanisa ya nyasi juu na chini, matope na juu majani, miti na juu mabati, matofari na juu mabati na vile ambavyo havina majengo bali waamini husali chini ya miti au wanatumia majengo ya shule. Kigango cha mwisho kipo umbali wa kilometa 60. Kigango hiki hupata huduma kipindi cha kiangazi kwa pikipiki tu. Parokia ina jumla ya waamini 5,679 kadili ya sensa ya 2017, na kati ya hao ni 1,500 walio hai. Mbali na changamoto hizo bado waamini wanaonekana kuhitaji wachungaji. Kwa sala na sadaka zetu tuendelee kushikamana ili utume huu kwa familia ya Mungu uweze kuleta matumaini na ndoto ya Mt. Gaspari iendelee kudhihirishwa kwa njia ya utume wetu. Mungu awabariki!

abt-img-02

abt-slider-01
abt-slider-01
abt-slider-01

Blessed are you, Virgin Mother! Your Son, Christ Jesus, spotless lamb has prepared for his spouse, the Church, the new bread and wine of the wedding banquet

Umebarikiwa, ee Mama na Bikira; Mwanao Yesu Kristo, Mwanakondoo asiye na doa, alilitayarishia Kanisa, mchumba wake, mkate na divai mpya ya karamu ya arusi

The cup of blessing that we bless is communion with the Blood of Christ. The bread that we break is communion with the body of Christ

(1Cor. 10:16)

Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je, si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, Je, si ushirika wa mwili wa Kristo?

(1Kor. 10:16)

Message From St. Gaspar

“I would rather die or suffer evil than to take such an oath. I cannot, I must not, I will not!” St. Gaspar spent five years in jail for refusing to take the oath"