“Our Congregation dedicates itself to the needs of the local and universal Church and devotes itself the Parrochial ministry and other works of the Apostolate which are assumed according to the Provincial, Vicariate and the norms of the Mission.” (NT S11)
OUR MISSION HOUSES
Below are our houses, click on the name to view
Katika mwaka wake wa Jubilei ya Dhahabu, Jimbo Katoliki la Singida limezindua Parokia mpya ya Mkiwa, na imekuwa Parokia ya thelathini katika Jimbo. Parokia mpya ya Mkiwa imewekwa chini ya ulinzi wa Mt. Ursula Ledochowska ambaye ni mwanzilishi wa Shirika la Masista wa Ursula wa Moyo Mt. wa Yesu Mteswa. Uzinduzi huo ulifanyika tarehe 27 Januari 2022, kwa Misa Takatifu iliyoongozwa na Mhashamu Baba Askofu Edward Mapunda wa Jimbo Katoliki Singida. Uzinduzi rasmi ulifanyika kwa kusoma hati maalum ya kuanzisha Parokia kadiri ya utaratibu unaoongozwa na Sheria za Kanisa (CCL # 515 ?1-3). Pd. Alessandro Manzi kwa barua ya uteuzi aliyomwandikia Baba Askofu, anakuwa Paroko wa kwanza wa Parokia ya Mkiwa. Pd. Alessandro alisimikwa kwa kiapo maalum na kukiri imani Katoliki mbele ya waamini. Wakili wa Askofu Pd. Francis Limu ndiye aliyesoma hati maalum ya kuisimika Parokia na kutaja mipaka yake na Vigango vinavyoiunda Parokia. Parokia ya Mkiwa inapakana kwa Kaskazini na Parokia ya Ikungi, mashariki inapakana na Parokia ya Manyoni, kwa kusini inapakana na Parokia ya Itigi, magharibi inapakana na Parokia ya Tura. Vigango vinavyoiunda Parokia ya Mkiwa ni Gurungu, Iwerewere, Weruweru na Choda.