MISSION HOUSES


“Our Congregation dedicates itself to the needs of the local and universal Church and devotes itself the Parrochial ministry and other works of the Apostolate which are assumed according to the Provincial, Vicariate and the norms of the Mission.” (NT S11)

Kisasa Parish

PAROKIA YA BIKIRA MARIA MAMA WA DAMU AZIZI YA YESU KISASA

                Awali waumini wa mwanzo wa parokia ya Kisasa walisali chini ya mti kabla ya kuzaliwa Kigango cha Mt. Anna. Baadaye waamini hao walijenga kibanda cha miti, na walipata huduma tokea parokia ya K/Ndege. Baada ya huduma kutoka parokia ya K/Ndege kusuasua hapo walianza kupata huduma tokea jimboni. Badaye waamini hao walihamishiwa parokia ya Mt. Gaspari- Makole baada ya kuwa parokia. Waamini hao wakiwa chini ya parokia ya Mt. Gaspari – Makole walipeleka ombi rasmi  kwa paroko wa Mt. Gaspari – Makole, Padre Adam Mbando ili aruhusu mapadre washirika la Damu Azizi kuwahudumia wakristo hao. Waamini hao waliendelea na jitihada zao katika imani na ilipofika mwaka 2004 walifanikiwa kupata huduma za kikanisa toka kwa mapadre wa damu Azizi hususani padre Reginald Mroso C.PP.S aliyekuwa mhimizaji na mwanzilishi wa jumuiya ya kwanza kwa waamini hao ijulikanayo kwa jina la Mt. Fransisko. Kanisa linalotumika mpaka sasa jiwe la msingi liliwekwa tarehe 04/01/2008 na kuzinduliwa rasmi tar 04/01/2010 na Mhashamu Baba Askofu Yuda Thadeus Ruwa’ichi, askofu wa jimbo la Dododma kwa wakati huo.

VIGANGO: Parokia ya Kisasa mpaka kufikia Julai 2020 ilikuwa na vigango vinne ambavyo ni; Kigango cha Mt. Anna- Medeli, Mt. Maria De Mathias- nyumba miatatu, Mt. Paulo wa mtume- Nzuguni maweni, na Kigango cha Mt Yohane mbatizaji- Nzuguni sokoine. Kuanzia Julai 2020 parokia imebakiwa na kigango kimoja cha Maria de Mathias, baada ya kigango cha Mt. Paulo wa mtume- Nzuguni maweni kuwa parokia teule na kukabidhiwa kwa mapadre wa jimbo la Dae es salaam, ambapo parokia hiyo teule ina vigango viwili. Parokia ya kisasa inajumuiya 24,na waamini wanaokadiriwa ni 1900 na Kigango cha Maria De Mathias kina jumuiya nne, na kinakadiriwa kuwa na waumini 300.

UONGOZI: Paroko wa kwanza wa parokia ya kisasa alikuwa Padre Richard Orota C.PP.S, na msaidizi wake alikuwa Padre Deusdedit Mulokozi, C.PP.S Mapadre hawa walitoa huduma mpaka mwaka 2012 mwezi Aprili. Baadaye padre Chesco Peter Msaga C.PP.S ambaye alikuwa Vicar General wa jimbo la Dodoma kwa muda huo alikaimu nafasi ya Paroko akisaidiwa na Padre Sostenes Ndendya C.PP.S ambao walikabidhi huduma kwa padre mpya Perfect Leiya C.PP.S tar 07/09/2014. Paroko wa pili ni Padre Perfect Leiya C.PP.S na msaidizi wake alikuwa padre Innocent Miku C.PP.S na baadaye Padre Sosthenes Ndendya C.PP.S ambaye amekabidhiwa kuwa paroko mpya wa Parokia ya kisasa mnamo tar 03/03/2019 akisaidiwa na padre Arcadius Mapinduzi C.PP.S.


Blessed are you, Virgin Mother! Your Son, Christ Jesus, spotless lamb has prepared for his spouse, the Church, the new bread and wine of the wedding banquet

Umebarikiwa, ee Mama na Bikira; Mwanao Yesu Kristo, Mwanakondoo asiye na doa, alilitayarishia Kanisa, mchumba wake, mkate na divai mpya ya karamu ya arusi

The cup of blessing that we bless is communion with the Blood of Christ. The bread that we break is communion with the body of Christ

(1Cor. 10:16)

Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je, si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, Je, si ushirika wa mwili wa Kristo?

(1Kor. 10:16)

Message From St. Gaspar

“I would rather die or suffer evil than to take such an oath. I cannot, I must not, I will not!” St. Gaspar spent five years in jail for refusing to take the oath"