Posted Mon Dec 2024
Post By : Fr.Felix Mushobozi
Mungu Mwenyezi, uliyeko katika ulimwengu wote na katika viumbe vyako vidogo zaidi, wewe unayezingira kila kitu kilichopo kwa huruma yako, mimina nguvu za upendo wako ndani yetu ili tutunze uhai na uzuri uliouumba. Tufurikishie amani, ili tuishi kama ndugu bila kumdhuru mtu yeyote. Ee Mungu wa maskini, utusaidie kuwakomboa walioachwa na kusahauliwa katika nchi hii ambayo ni ya thamani sana machoni pako. Ponya maisha yetu, ili tuulinde ulimwengu na sio kuupora, ili tupande uzuri na sio uchafuzi wa mazingira na uharibifu.
Posted Sat Dec 2024
Post By : Fr.Felix Mushobozi
Ee Mungu wangu, nijalie niweze kutambua thamani ya neema hii uliyonipa. Wito huu ulionipa ni chemchemi ya neema zingine zote. Umeniita niache ndugu zangu, rafiki zangu na starehe nyingine za dunia. Uwe kiongozi wa moyo wangu, niambatane nawe daima. Nakuomba na kukusihi dhambi zangu zisiwe kizuizi cha kupata huruma yako.
Kwa msaada wa neema yako, naahidi kuwa mwema, mwaminifu na mtiifu katika kutimiza mapenzi yako katika kila jambo. Najua, utanifanya kuwa mtakatifu, kwa hilo usifiwe mara elfu. Maisha yangu yote ni yako, nayatolea yote kwako; nataka kuwa wako, unitendee unavyotaka.
Nakubali majaribu, usumbufu, uchungu, taabu, magonjwa na lolote litakalonipata. Ee Mungu unipe upendo mkubwa, niishi maisha ya kukupenda wewe daima, mpaka kifo changu.
Lakini Yesu, sisali kwa ajili yangu tu. Ninalo deni kubwa kwa shirika hili lililonikaribisha, kunipokea na kunitunza. Ni kwa jinsi gani nitaweza kulitumikia inavyostahili! Ee Bwana lilinde na kuliimarisha, listawishe, liwe na upendo na lidumu daima katika mwanga wa Roho wako Mtakatifu. Shirika lipate kuzidisha huduma zake popote pale linapohitajika. Mpe kila mwanashirika mahitaji yake ya kiroho na kimwili. Waongoze viongozi wake ili watimize mipango yako tu. Mwaga baraka nyingi kwa wafadhili wetu. Bariki kazi na mipango ifanywayo na shirika ili izae matunda kwa watu wote.
Nakutolea pia vyama na jumuiya zote zinazotoa heshima kwa Damu yako Azizi, ili kazi zao zizae matunda kwa ajili ya wote. Ee Damu Takatifu ya Yesu ongeza nguvu ya sala.
Maria Mtakatifu, kwa maombezi yako tutapata amani ya mwili na roho na maisha bora ya milele. Enyi malaika wote wa mbinguni, hasa malaika mlinzi wangu, fikisha maombi yangu kwa Yesu na Maria ili kwa huruma yao, yapate kusikilizwa. Mtakatifu Fransisko Xaveri, Watakatifu wote wa mbinguni, liombeeni Shirika, wanashirika wote na mimi mwenyewe, Amina!
Posted Fri Jul 2022
Post By : Fr.Felix Mushobozi
It is an incontestable that the most Blessed Sacrament should be the center of our hearts. The sacred Ciborium is the wine cellar wherein Jesus cuptures our affections and draws us to Himself!! (St. Gaspar # 2177).
Posted 0000-00-00
Post By : Admin
Impelled by the mission of the Church and by the charism of St. Gaspar, the Missionaries of the Precious Blood of the Italian Province began the mission of Tanzania in 1966. In 1972 it became a delegation with its own regulations. Thanks to the increase of the members and of charitable and apostolic works it was elevated to a Vicariate on July 27, 1998. It continued to grow and on August 8, 2015, it was elevated to the status of a Province.
The Province of Tanzania of the Society of the Precious Blood is governed by its own Statutes. These Statutes govern the authority of the assemblies, of the Provincial Director and his Council, and everything else that concerns the Province.