Posted 2024-02-19 05:10:14

Post By : Fr.Felix Mushobozi

WAMISIONARI KUMI NA MMOJA WAPEWA DARAJA LA UPADRE NA MMOJA DARAJA LA USHEMASI

Jumamosi Januari 13 mwaka huu, Wamisionari kumi na moja walipewa daraja la Upadre na Mseminari mmoja daraja la Ushemasi. Tukio hilo la kihistoria lilifanyika Dodoma katika Parokia ya Malkia wa Damu Azizi - Kisasa. Askofu Mkuu Beatus Kinyaiya Mkuu wa OFM, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma ndiye aliyetoa madaraja hayo. Wafuatao ndio waliopewa daraja la Upadre: Shemasi Abelhad Ismail Dimosso Mzaliwa wa Tegetero Morogoro; Shemasi Aidan Alphonce Mtui Mzaliwa wa Mbahe Aris Moshi; Shemasi Abibon Lawrent Rukiza Mzaliwa wa Kemondo Bukoba; Shemasi Appolonius Ludovick Byarugaba Mzaliwa wa Nshamba Kagera; Shemasi Bonaventure Aquiline Maro Mzaliwa wa Kishimundu Moshi; Shemasi Ernest August Shirima Mzaliwa wa Tarakea Rombo Kilimanjaro; Shemasi Gregory Ndeshillo Mzaliwa wa Mrao Rombo Kilimanjaro; Shemasi James Titus Makinda Mzaliwa wa K/Ndege Dodoma; Shemasi Joseph Richard Msumeno Mzaliwa wa Kambikatoto Chunya Mbeya; Shemasi Livinus Ndamwesiga Benedicto Mzaliwa wa Maruku Bukoba na Shemasi Revocatus Charles Gimbuya Mzaliwa wa Chamgasa Simiyu.

Mseminari aliyepewa daraja la Ushemasi siku hiyo ni Wilbrant Clodi Urio ambaye alipokelewa Shirikani rasmi na kwa daima siku ya Ijumaa Januari 12, siku moja kabla ya kupewa Ushemasi. Kwa hakika tukio hili ni la kihistoria kwa idadi ya waliopewa daraja takatifu. Idadi kubwa kama hii ilishuhudiwa kwa mara ya mwisho mwaka 2003 ambapo iliyokuwa Vikarieti ya Tanzania wa wakati huo ilishangilia idadi ya Wanashirika kumi na mmoja wakipewa daraja la Upadre mwaka huo. Katika tukio hilo hilo Wanashirika watatu wa Stigmatine walipewa daraja la Ushemasi pamoja na Shemasi Wilbrant Clodi Urio.

Baada ya kuwekwa wakfu kila padre alikwenda katika parokia yake ya nyumbani kwa ajili ya misa yake ya shukrani. Kwa sababu ya umbali kutoka sehemu moja hadi nyingine vikundi vitatu viliundwa kulingana na mikoa ya nchi ili kuwezesha ushiriki wa wanashirika wengine katika sherehe hizo.

Siku hiyo hiyo Mkuu wa Province aliwatangazia sehemu zao za Utume kama ifuatavyo:

Abelhad Ismail Dimosso – Parokia ya Mkiwa; Aidan Alphonce Mtui – John Merlini Formation House; Abibon Lawrent Rukiza – Teutonic Province; Appolonius Ludovick Byarugaba – Parokia ya Old Maswa; Bonaventure Aquiline Maro - Roma kwa masomo ya tasnia ya Mawasiliano; Ernest August Shirima – Parokia ya Shanwe Mpanda; Gregory Ndeshillo – Parokia ya Mkula Ifakara; James Titus Makinda – Masomo ya tasnia ya Mawasiliano SAUT; Joseph Richard Msumeno Parokia ya Kinda na Nyumba ya Malezi; Livinus Ndamwesiga Benedicto – Parokia ya Manyoni; Revocatus Charles - Utume Teutonic Province. Shemasi mpya Wilbrant Urio amepangiwa Parokia ya Manyoni ambako Jimbo la Singida linaandaa Vigango vinne kuwa Parokia.

blog-img