Posted 2020-03-14 07:14:52

Post By : Admin

MSHAURI WA SHIRIKA ULIMWENGUNI AJIUZURU

Mnamo tarehe 26 Februari mwaka huu, Fr. Augusto Menichelli, C.PP.S. ambaye ndiye alikuwa Mshauri wa pili katika Halmashauri ya Shirika Ulimwenguni alimkabidhi Mkuu wetu wa Shirika barua ya kujiuzuru kwa sababu za afya. Mkuu wetu wa Shirika Ulimwenguni ameandika barua kwa wanashirika wote akituomba tumwombee Pd. Augusto katika kipindi hiki anaposhughulikia afya yake aweze kupona na kurudi katika utume wake kwenye Provinsi yake ya Atlantic.

Kadiri ya miongozi ya kikatiba ya Shirika, Mkuu wa Shirika hufanya kazi yake akishirikiana na Halmashauri wanne; na ikitokea mmoja wapo akalazimika kuachia nafasi yake, Mkuu wa Shirika na washauri waliobaki huchagua atakayeshika nafasi yake kati ya wale ambao katika uchaguzi mkuu uliomchagua aliyetoka walipata kura nyingi zaidi Rej. NT S31 & 31.

blog-img